KUELEKEA MSIMU MPYA WA LIGI KUU BARA MWADUI YAIFUMUA PAMBA 5-3 NYAMAGANA
KATIKA kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mwadui FC leo imeteremka Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza na kumenyana na wenyeji, Pamba FC katika mchezo wa kirafiki.
Katika mchezo huo, Mwadui FC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Pamba inayojiandaa na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara nayo.
Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Salim Khamis, Awadh Juma kila mmoja mawili na lingine Nyanda Babi, wakati ya Pamba yamefungwa na Peter Magata, Meshack Kikona kwa penalti na Peter Aguero.
No comments