Header Ads

SANCHEZ ANAHAMA ARSENAL, HUKU MAN CITY IKIKUBALKI KUMTOA STERLING NA PESA

Image result for SANCHEZ
Manchester City wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya kumnasa Alexis Sanchez kutoka Arsenal wiki hii, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.

City wameonyesha nia kubwa sana ya kutaka kumnasa Sanchez kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya Alhamisi.

Chombo kimoja cha habari cha nchini Chile, T13  kimearifu kwamba Sanchez ameomba ruhusa ya kuondoka katika kambi ya timu ya taifa ya Chile ili kwenda 'kufanya biashara zake binfasi'.

Chanzo kimoja kutoka City kimeiarifu Sky Sports kwamba City wapo tayari kumjumuisha Raheem Sterling sehemu ya dili hilo.

Sky Sports wameambiwa kwamba Sanchez hana furaha katika kikosi cha Arsenal na anataka kuondoka.

No comments

Powered by Blogger.