Header Ads

GOTI LAMPELEKA INDIA KIPA BORA WA COSAFA.

Taarifa kutoka katika idara ya habari ya Simba zinasema kuwa mlinda mlango nambari mbili wa klabu hiyo Said Mohamed maarufu kama Nduda ameumia goti na atapelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi. Simba kuptia msemaji wake Haji Sunday Manara wamedai kuwa Nduda aliumia wakati wa maandalizi ya Mechi ya Ngao Ya Jamii dhidi ya Yanga hivyo kumfanya kukosa mechi hiyo.


Aidha Manara amesema kuwa mlinda mlango huyo ambaye ni kipa bora wa michuano ya COSAFA atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne hadi sita wakati akiwa anapata matibabu. Manara aliongeza kuwa Beki wa pembeni wa klabu hiyo Shomari Kapombe anarejea uwanja hivi karibuni na Haruna Niyonzima naye ameanza kufanya mazoezi na wenzake kambini.


No comments

Powered by Blogger.