Header Ads

WAZIRI NCHEMBA AMELIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAKAMATA BODABODA WENYE MAKOSA HAYA

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi  Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la polisi nchini kuwakamata wamiliki wapikipiki ambao watashindwa kuwa na kofia ngumu za pikipiki maarufu kama bodaboda. 

Waziri Mwigulu ameyaongea hayo wakati akiongea na madareva wa pikipiki wa wilaya ya Shinyanga ambao wanapatiwa mafunzo ya usalama barabarani mkoani humo ambapo amewataka polisi wakiwakamata madereva wa pikipiki wakiwa hawana kofia ngumu wawaulize mmiliki wake ni nani ili naye akamatwe aulizwe kwanini hana kofia ngumu na awekwe ndani. 

Waziri Mwigulu amesema pia kama abiria naye akikataa kuvaa kofia ngumu na wakati pikipiki ina kofia hizo basi naye akamatwe na dereva pikipiki achiwe aendelee na biashara kwani kila mtu lazima atimize wajibu wake hivyo anatoa mwezi mmoja madereva wote wa pikipiki na wamiliki wahakikishe wanakofia ngumu mbili za pikipiki.
 
Naye mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Steven Masele amesema zamani palikuwa na msuguano mkubwa sana kati ya madereva wa pikipiki na askari wa jeshi la polisi hali iliyopelekea kutokuwa na mahusiano mazuri kati yao lakini kwa sasa mahusiano ni mazuri na yanaridhisha kutokana na juhudi zilizojengwa na RPC mpya.
 

Kamanda wa Polisi mkoani wa shinyanga ACP Simon Haule amesema mafunzo hayo ni utekelezaji wa maagizo na mkuu wa mkoa baada ya wananchi wengi kutojua au kutokutumia sheria ya matumizi ya barabara hasa katika mzunguko ( roundabout).

No comments

Powered by Blogger.