Header Ads

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKUWAFUMBIA MACHO WALA RUSHWA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa TAKUKURU katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema kuna mambo mengi ya ovyo yanayofanyika, na ktolea mfano wa uhakiki uliobaini pembejeo za ruzuku zenye madai ya Shilingi Bilioni 48 hewa, wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, kaya masikini hewa 56,000 zilizopaswa kupata fedha TASAF na wanafunzi hewa 5,850 waliotakiwa kupata mkopo.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Angela Kairuki, Rais Magufuli amesema ana imani na TAKUKURU na amewataka wafanyakazi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu mkubwa na kwamba Serikali itafanyia kazi changamoto zinazowakabili.

No comments

Powered by Blogger.