Header Ads

MAWAKILI MWANZA HAWAJAELEWANA WAPO WALIOGOMA WAPO WALIOSUSIA MGOMO.


Chama cha Mawakili Tanganyika TLS kupitia kwa Rais wake Tundu Lissu kilitangaza mgomo wa siku mbili kususia shughuli za Mahakama kuwaunga mkono Mawakili wa IMMMA Advocates kufuatia Ofisi zao kuvamiwa na kulipuliwa.

Hali ya sintofahamu imeendelea miongoni mwa Mawakili katika Mkoa wa Mwanza ambao pia ni Wanachama wa Chama hicho ambapo kumekuwa na mgawanyiko huku baadhi wakiunga mkono na kususia shughuli za Mahakama lakini wengine wakionesha kupinga hatua hiyo na kuendelea na shughuli za Mahakama kama kawaida kwa sababu mbalimbali.

No comments

Powered by Blogger.