Header Ads

LICHA YA IBRAHIMOVIC KUSAINI MAN UTD ITABIDI ASUBIRI HADI... POGBA NAYE...



Zlatan Ibrahimovich ameshasaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kukipiga na Manchester United usajili ambao mashabiki wa United wameufurahia na kuchekelea sana.
Lakini kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameeleza kwamba mshambuliaji huyo hatakuwa na mashetani hao wekundu uwanjani hadi mwaka 2018 ambapo ligi itakuwa katika raundi ya pili.
Mourinho hataki Kadabra apate tabu bali anataka awe na muda mrefu nje ya uwanja ili aendelee kuuguza majeraha yake na akiwa fiti 100% ndio atarejea katika kikosi hicho cha mashetani wekundu.
“Atakuwa mchezaji wetu wa ziada katika raundi ijayo ya ligi, nikisema raundi ijayo namaanisha mwaka 2018, nataka apate muda wa kuwa imara zaidi na naamini hadi baada ya msimu wa Christmas atarejea uwanjani” alisema Mourinho.
Jose Mourinho amesema wataweka jina la Zlatan Ibrahimovich katika orodha ya wachezaji wao wanaokwenda kupambana katika michuano ya Champions League msimu huu lakini akasema hana uhakika kama Kadabra atakuwepo katika michezo ya makundi.
“Hatutaki kumuacha mchezaji yoyote katika kikosi chetu cha Champions League na yeye jina lake litakuwepo lakini nadhani hatakuwepo hatua ya makundi labda hadi ikifika katika hatua ya mtoano” alisema Mourinho ambaye team yake ipo kundi moja na Benfica,Cska Moscow na Basel katika michuano hiyo.
Katika habari nyingine kutoka OT ni kwamba kiungo wao Paul Pogba ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Europa League akiwabwaga Zlatan Ibrahimovich na Henrikh Mkhitaryan.

No comments

Powered by Blogger.