Header Ads

BOMOABOMOA INAYOENDELEA MTAA WA SINZA LEGHO.


Kilio cha bomoabomoa, asubuhi hii kimehamia Sinza Legho jijini Dar es Salaam ambapo jengo ambalo zamani lilikuwa likifahamika kama 92 Club, ambalo baadaye lilibadilishwa matumizi na kuwa kanisa na maduka ya biashara mbalimbali, limebomolewa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mgogoro wa umiliki.





Bomoabomoa hiyo imeanza alfajiri ambapo wahusika wakiwa hawana taarifa juu ya kinachoendelea, walishtukia kundi la watu likianza kuvunja jengo hilo kabla ya baadaye tingatinga kuwasili na kumaliza kazi, ambapo hakuna aliyeruhusiwa kutoa kitu chochote.

No comments

Powered by Blogger.