Header Ads

SIMBA YATANGAZA UBAYA LIGI KUU BARA YAPIGA MTU 7 - 0, MATOKEO MENGINE YA MECHI ZA LEO NIMEKUWEKEA PIA.


Pazia la ligi kuu Vodacom Tanzania bara limefunguliwa leo, huku ikishuhudiwa nyasi za  viwanja mbalimbali nchini vikiwaka moto, klabu ya soka ya Simba ambayo msimu huu imefanya usajili wa kihistoria imeanza ligi hiyo vema kwa kushusha kipigo cha mbwa mwizi kwa Ruvu Shooting ya Massau Bwire kutoka mkoani Pwani, kwa kuilaza magoli 7 - 0, katika dimba la uhuru jijini Dar es salaam,
Emmanuel Okwi ndiye liyefungua karamu ya  magoli katika dakika ya 18 akimchambua kipa Bidii Hussein baada ya pasi ya Muzamir Yassin na goli la pili lakafunga dakika ya 22 baada ya kuwachambua mabeki ndani ya kumi na nanebaada ya kupokea majaro safi kutoka kwa  kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

.
Baadaye Okwi akafunga goli la 3, na kumfanya kupiga hat trickdakika ya 35 baada ya pasi nzuri ya Muzamir Yassin  tena kabla ya kusaidia kupatikana kwa bao la nne.

Okwi aliwatoka wachezaji wa Ruvu Shoting hadi karibu na boksi na kumpasia beki Erasto Nyoni pembeni kushoto, aliyetia krosi iliyosindikizwa nyavuni na winga machachari, Shiza Kichuya kuipatia Simba bao la nne dakika ya 42.

Mshambuliaji wa zamani wa Zesco United ya Zambia, Juma Luizio Ndanda akaifungia Simba bao la tano dakika ya 44 akimalizia krosi ya Nyoni, kabla ya Okwi kufunga bao lake la nne leo na la sita katika mchezo dakika ya 52 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo Saidi Hamisi Ndemla.
Beki aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC baada ya kusajiliwa kutoka Azam FC, Erasto Edward Nyoni akakamilisha shangwe za mabao za Wekundu wa Msimbazi kwa kufunga la saba dakika ya 81.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu katika siku ya kwanza ya ufunguzi leo ni; Mwadui imeshinda 2-1 dhidi ya Singida United Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Mtibwa Sugar wameilaza 1-0 Stand United Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Azam FC imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi, Yanga SC kuikaribisha Lipuli ya Iringa Uwanja wa Uhuru.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Ally Shomary, Erasto Nyoni, Method Mwanjali/Juuko Murshid dk65, Salim Mbonde, James Kotei, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk46, Juma Luizio, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk43.

Ruvu Shooting; Bidii Abdallah, Said Madega/Amani George dk50, Yussuf Ngunya, Shaibu Nayopa, Mangasini Mbonosi, Baraka Mtui, Chande Magoja, Shaaban Msala, Ishara Said, Jamal Mtegeta na Khamis Mcha ‘Vialli’/Said Dilunga dk46.

1 comment:

Powered by Blogger.