Header Ads

BREAKING NEWS:AJALI ,DALADALA IMEGONGANA NA TRENI MOROGORO MJINI,WATU KADHAA WAMEFARIKI


Habari kutoka Mkoani Morogoro zinasema kuna ajali imetokea maeneo ya Tanesco mjini Morogoro ambapo Gari /Daladala imegongana na Treni.

Kwa mujibu wa ripota wetu Ndugu Erneo Gwandiko ambae alifika katika eneo la tukio amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuhi ya leo Agosti 23.

Treni hiyo  ilikuwa ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam

Inasemekana kuwa kuna watu kadhaa wamefariki kutokana na ajali hiyo lakini bado haijajulikana idadi yao.

Dereva wa dalala ambao ameonekana kuwa chanzo cha ajali hiyo amekimbia kusikojulikana.

Majeruhi na waliofariki wamepelekwa katika hospitali yamkoa wa morogoro

Taarifa kamili tukuletea hapo baadae
  

No comments

Powered by Blogger.