Header Ads

HUYU NDIYE TSHISHIMBI WA YANGA ALIYEKUWA NYOTA KWENYE MCHEZO WA JANA


Kiungo mpya wa Yanga Papy Kabamba tshishimbi amekuwa gumzo kila kona nchini kutokana na kiwango kizuri alichokionesha kwenye mchezo wa jana dhidi ya Simba.

Ni mechi ya kwanza kwa kiungo huyu mkabaji wa Yanga SC aliesajiliwa kutokea Mbabane Swallows ya Swaziland . 

Kwa kiasi kikubwa ndio alikuwa akivunja mipango yote ya Simba eneo la kati . Ameonesha mchezo mzuri kwenye mechi yake ya kwanza na Yanga . Aliweza kuwalinda vyema walinzi wa kati , kujenga muunganiko mzuri na kiungo wa juu Kamusoko pia kuwachezesha Ajibu na switching za kulia na kushoto kwa Martin na Rafael Daudi.

Baadhi ya watu waliokunwa na kiwango cha Tshishimbi ni pamoja na mtangazaji wa vipindi vya michezo vya Radio EFM,Oscar oscar akiwa ameandika maneo yafuataoyo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

 "Kama kuna RASTA mwingine amebakia huko Kusini Mwa Jangwa la Sahara, Yanga wakamsajili tu. Kamusoko alishaeleweka, sasa ni Tshishimbi. CLASS"

No comments

Powered by Blogger.