NYUMA YA PAZIA: WACHEZAJI BORA 11 WANAOUNDA KIKOSI CHA KWANZA NGAO YA JAMII.
Shaaban
Maulidi #MaulidiTV
Mchezo wa kandanda ndiyo
mchezo unaopendwa na watu wengi zaidi duniani na hapa Tanzania bila shaka
mchezo huu ndiyo unaopendwa zaidi. Lakini mapenzi yanazidiana na hii haimaanishi
tu kila timu inayosakata kabumbu basi ndiyo ipendwe sawa na nyingine.
Kwa hapa Tanzania
unapozungumzia soka basi huwezi kuacha kuzitaja klabu za Simba na Yanga ambazo
zimebeba jina na uzito wa kandanda la Tanzania. Siku ya Jumatano Agosti 23 2017,
timu hizi zilikutana katika dimba la Taifa kupepetana ili kuweza kulichukua
taji la Ngao Ya Jamii, ambalo muhimu
katika kuweka rekodi zao vizuri.
Hapa nimekuwekea idadi ya
wachezaji 11 wanaounda kikosi cha kwanza katika pambano hilo, kulingana na
kiwango cha uchezaji waliokionesha lakini yote kwa yote ni kwa mtazamo na maono
ya mwandishi wa Makala hii.
1. AISH MANULA.
Kwanza huyu ndiye Mlinda
mlango nambari moja kwa Timu ya Taifa ya Tanzania kwa sasa. Amesajiliwa na Simba
akitokea Azam ambako amelelewa na kucheza kwa muda mrefu. Ni kijana mdogo ambaye
ni hazina kubwa ya taifa mathalani katika ulimwengu wa soka. Katika mchezo wa
ngao ya jamii ameonesha na kudhihirisha ni kwa nini mwalimu wa kikosi cha timu
ya taifa kumwamini na kumfanya mlinda mlngo nambari moja, pia maeonesha thamani
ya usajili wake Simba. Ameokoa michomo ya hapa na pale japo hakupata kashikashi
za kutoka. Ameoangua penalti ya kwanza na kuisadia klabu yake kuibuka mshindi.
2. ALLY SHOMARI
Kijana aliyesajiliwa
akitokea Manungu Tuliani mkoani Morogoro alipokuwa akikipiga na wakata miwa wa
Mtibwa Sukari. Hakuna aliyetarajia kuwa
ataanza lakini huenda kutokuwepo kwa Shomari Kapombe kulimpa nafasi ya kucheza.
Ameonesha kiwango kizuri cha kukaba wachezaji wazuri wa Yanga lakini aliweza
kupandisha mashambulizi. Anaonekana ni mwenye kutumia akili na nguvu pia.
3. GADIEL MICHAEL.
Atakumbukwa sana na
wapenzi na mashabiki wa timu ya Azam, lakini kwa sasa ni mchezaji wa Yanga.
Kijana huyu ni mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu lakini vilevile ana
kiapji kikubwa. Amecheza vizuri katika nafasi yake na kuwafanya kina Okwi na
KIchuya kushindwa kuwika lakini pia uwezo wake wa kupandisha mashambulizi
kunamfa kuwa bora zaidi.
4. SALUM MBONDE
Ni mchezaji mwingine
kutokea Mtibwa Sikari aliyesajiliwa Simba msimu huu. Ana akili sana anapokuwa
uwanjani ana usafi wa matendo, utulivu wake pia humpamba zaidi na kumfanya
aoanekane bora kuliko wenzake uwanjani. Kwa siku ya jana ameonesha kiwango
kizuri hivyo natshili kuwemo katika kikozi cha kwanza.
5. METHOD MWANJALE.
Wenyewe wanamwita baba
mwenye nyumba, uzoefu wake, akili, nguvu na ukomavu wake ndivyo vimefanya
akwepe panga la kutemwa licha majeruhi yaliyokuwa yakimsibu. Mwanjale kwa jana
ameonesha kiwango kikubwa sana na anastahili kuwemo pia katika kiosi hiki.
6. PAPPY KABAMBA TSHISHIMBI.
Sio mwenyeji sana lakini
jina lake kwa sasa ni maarufu sana, amefanya mazoezi na Yanga kwa muda mchache
lakini kwa kiwango alichokionesha jana si haba. Ana jicho lakuuona mpira,
anakaba, anatoa pasi nzuri zenye macho na alifanikiwa kabisa kuituliza timu ya
Yanga. Huyu ndiye anastahili kuitwa
Nyota wa Mchezo.
7.
SHIZA
KICHUYA.
Hapa hakuna mwenye swali
la kwa nini bwana mdogo huyu mwenye maajabu ya kipekee katika soka hasa la
Tanzania. Kichuya atakumbukwa milele kwa goli la kona ya moja kwa moja lakini
lile lililomfanya achukue tuzo ya goli bora la Msimu wa 2016/2017 siku ya jana
pia alikuwa katika ubora wake.
8. MZAMIRU YASSIN
Huyu jamaa uwanjani huwa
kama hayupo vile, lakini inapokuja suala la tathmini basi inakuwa ni vigumu
sana kumuacha. Amecheza vizuri sana na anafaa kuwa katika kikosi hiki kwani
uwezo wake kwa siku ya jana ulikuwa ni wa kiasi kikubwa mno.
9. IBRAHIM AJIB
Wengi watauliza kwa nini
yupo katika nafasi hii lakini ukweli ni kwamba Ajib ndye mshambuliaji aliyeonesha
kiwango kikubwa katika pambano la jana hivyo anatashili kuwemo na kuwa katika
nafasi hii. Haji Sunday Manara aliwahi kusema ya kuwa “ukiwaacha Diamond na
Alikiba binadamu pekee anayetoa burudani ya hali ya juu ni kijana huyu”. Kuhama
kwake Simba hakumfanyi kuwa ameshuka kiwango bali ubora wa Ajib unafahamika
hadi kwa yule mtoto mdogo aliyechora shati lake namba na jina la Ajib.
10. EMMANUL OKWI
Unaweza kumuita mfalme wa
Simba kama mabavyo wenyewe wanamuita. Amekuwa kipenzi cha wapenda soka kwa aina
ya uchezaji wake na msaada wake katika timu. Siku ya jana aliweza kucheza
vizuri sana kiasi cha kutosha kuonekana katika orodha hii.
11. HARUNA NIYONZIMA.
Huyu ndiye Fabregas wa
Afrika Mashariki, jina hili hakupewa kwa sababu ya kufanana kwa sura na yule kiungo
wa Chelsea Cesc Fabregas la hasha, bali ni kwa aina ya uchezaji wake. Pasi zaake
murua, chenga na kujituma mdiko kumemfanya aweze kuingia katika oroidha hii.
Tupe maoni yako hapa.
No comments