Header Ads

DEMBELE AMEWEKA REKODI HII KWA KUTUA BARCELONA KWA DAU HILI.


Klabu ya Barcelona imetangaza kumsajili kiungo mshambuliaji Ousman Dembele kwa ada ya pauni milioni 96 kutoka Borrusia Dortmund ya Ujerumani.

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa anakuwa mchezaji ghali zaidi chipukizi kusajiliwa kwa dau kubwa, ametua kikosini hapo kuchukua nafasi ya Neymar ambaye amesajiliwa na Paris Saint-Germain.

Atasaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na timu hiyo Jumatatu na atakabidhiwa jezi namba 11 iliyokuwa ikivaliwa na Neymar.

No comments

Powered by Blogger.