Header Ads

MABINGWA WATETEZI YANGA WAMEANZA KWA SARE HII DHIDI YA LIPULI FC.


Baada ya kushuhudiwa pazia la ligi kuu bara likifunguliwa hapo jana. Leo Ligi hiyo imeendelea pale katika dimba la Uhuru ambapo ilizikutanisha Klabu ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wakimenyana vikali na Timu ya Lipuli FC, iliyopanda daraja msimu huu.
Mchezo huo umemalizika kwa sare ya goli 1 – 1, huku ikiwalazimu Yanga  kusawazisha goli hilo mwishoni kabisa mwa kipindi cha kwanza. Lipuli ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Seif Karihe na Yanga wakasawazisha kupitia Donald Ngoma katika dakika za nyongeza za Mchezo huo. Magoli hayo yalidumu hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi kunalia.

No comments

Powered by Blogger.