Header Ads

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA KIGAMBONI LEO, AJICHANGANYA NA WANANCHI KWENYE PANTONI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akigongesheana tano na mmoja wa vijana aliokuwa anavuka nao kutoka Magogoni kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam kwa pantoni ya MV Kigamboni alipofanya ziara ya ghafla huko

  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiongea na mmoja wa abiria aliokuwa anavuka nao kutoka Magogoni kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam kwa pantoni ya MV Kigamboni alipofanya ziara ya ghafla huko

Rais Magufuli atembelea eneo la Feri Jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo. Avuka kwa kutumia kivuko cha MV Kigamboni Kutoka Magogoni kwenda Kigamboni.

Rais baada ya kushuka ameongea na baadhi ya wananchi wa Kigamboni kuwaahidi kushughulikia changamoto zao, wananchi pia wamepata nafasi ya kuuliza maswali;

=>Rais Magufuli: Serikali ninayoingoza itakuwa ya watu wote bila kubagua vyama, dini, makabila na mimi ni rais wa watanzania wote.

=>Nitawa-instruct watu wangu mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, wakurugenzi ili yote yafanyiwe kazi.

=>Tumeamua kuunda agent nyingine ya barabara ambayo itashughulikia barabara za halmashauri.

No comments

Powered by Blogger.