Header Ads

Treni zenye kasi zaidi dunia kusafiri kwa kilomita 300 kwa saa China

Treni za mwendo kasi zaidi kuzinduliwa nchini China
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captiTreni za mwendo kasi zaidi kuzinduliwa nchini China
Treni za mwendo kasi za China sasa zinatarajiwa kuwa na kasi zaidi duniani.
Kasi ya juu ya treni ya kisasa nchini China ilikuwa kilomita 300 kwa saa mwaka 2011 kufuatia ajali mbili ambazo ziliwaua takriban watu 40.
Kuanzia wiki ijayo baadhi ya treni hizo sasa zitaruhusiwa kwenda kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa.
Kasi hiyo ya juu inalenga kupunguza muda wa saa moja kati ya Beijing hadi Shanghai.
Kufikia tarehe 21 mwezi Septemba, treni saba za mwendo kasi nchini China zitaruhusiwa kusafiri kwa kasi hiyo ilioongezwa.
Ili kuadhimisha kurudi tena kwa treni mwendo kasi, treni hizo sasa zitaitwa ''Fuxing' ama ''zilizoimarishwa'.
Treni zote zimewekwa mfumo ulioimarishwa ambao utapunguza kasi ya treni hizo na kuzisimamisha iwapo kutakuwa na dharura .
Shirika la treni nchini China linaaminika kutafuta njia za kuimarisha reli ili kusaidia treni hizo kusafiri kwa mwendo wa kasi zaidi wa hadi kilomita 400 kwa saa.
China inadaiwa kuwa na takriban kilomita 19,960 ya reli ya mwendo kasi.
Ajali ya 2011 ya treni mwendo kasi ilisababisha uchunguzi kufanywa hatua iliogundua kuhusu ufisadi mkubwa katika wizara ya reli.
Uchunguzi huo ulisababisha maafisa wengi kushtakiwa kwa ufisadi na utumizi mbaya wa madaraka.
Maafisa wawili waandamizi walihukumiwa kunyongwa.

No comments

Powered by Blogger.