NYUMA YA PAZIA: LICHA YA SIMBA KUCHUKUA UBINGWA LAKINI LAZIMA WAZINGATIE HAYA.
Siku ya jana ni muhimu
pengine pengine kuliko siku za hivi karibuni kwa klabu ya Simba. Umuhimu wake
hapa si wa kuchukua ubngwa wa Ngao ya Jamii, bali nikuchukua kikombe mbele ya
mahasimu wao wa jadi yaani Yanga tena kwa kuwafunga.
Macho na masikio ya watanzania
wengi yalielekezwa pale wilayani Temeke katika dimba la taifa lililokaribiana
kabisa na Chuo Kikuu Kishiriki Cha Cha Elimu Dar es salaam (DUCE), ambapo
watani wa jadi Simba na Yanga walikuwa wakipepetana vikali.
Kabla ya kuanza kwa
pambano hilo kulikuwa na tambo za hapa na pale wakati Haji Sunday Manara
akiwaandaa mashabaiki na wapenzi wa Klabu hiyo kuwa Yanga lazima afe si chini
ya goli 5, Salum Mkemi yeye akizungumza dakika chache kabla ya pambano kuanza
aliwaonya mahasimu wao Simba kuwa matokeo waliokuja nayo mikononi wayaache
wsubiri dakika 90.
Kwa kuwa siku hazigandi
basi hata muda nao hausimami, hatimaye lile pambano lililokuwa likisubiriwa kwa
hamu likaanza mnamo majira ya saa 11: 00 za jioni. Simba inayonolewa na Joseph
Omog iliwaanzisha Aishi Manula, Ally Shomari, Erasto Nyoni, Salum Mbonde,
Method Mwanjale, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Emmanuel Okwi na
Haruna Niyonzima. Yanga waliwaanzisha Rostand Youthe, Juma Abdul, Gadiel
Michael, Andrew Vicent, Kelvin Yondani, Pappy Tshishimbi, Emmanul Martine,
Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Ibrahim Ajib na Raphael Daud.
Mchezo ulikuwa mzuri
kiasi chake lakini haukuwa na ladha ambayo tuliambiwa na kuitegemea hivhyo
kuufanya uwe wa kawaida kama alivyotabiri Massau Bwire. Baada ya dakika 90
kukamilika kwa sare tasa ya bila kufungana ndipo ilipomlazimu mwamuzi Elly
Sassy kulipeleka pambano hilo kuamuliwa kwa changamoto ya Mikwaju ya penalti huku
Simba ikiibuka na ushindi wa penalti 5 – 4 za Yanga.
Simba wanastahili pongezi
kwa hili lakini jambo la kuzingatia ni kwamba bado safu yao ya ushambuliaji
inayoongozwa na Laudit Mavugo bado ni butu huku ikishindwa kuzifumani nyavu za
timu pinzani. Ikumbukwe ya kuwa msimu uliomalizika Simba ilikosa taji la ligi
kuu ambalo kwa miaka kadhaa imekuwa ikilisotea lakini wakalikosa kwa tofauti ya
idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa na kuwaacha Yanga wao waliokuwa na
hazina ya kutosha ya magoli kulichukua kombe hilo mara tatu mfululizo.
Nilichokiona kwa Mavugo si
mchezaji wa kubezwa hata kidogo tena naweza kuthubutu kusema ya kuwa huyu ndiye
mshambuliaji bora kwa sasa, lakini jambo ambalo mwalimu Omog anatakiwa
alizingatie ni namna ya kumtumia mchezaji huyu kwani amekuwa akikosa utulivu
pia amekuwa akihama mara kwa mara kwenye nafasi yake hivyo kuwaacha mabeki
wakiwa huru bila ya kash kash ya hapa na pale. Kama atapata utulivu huku Shiza
Kichuya na Emmanuel Okwi na Niyonzima wakijua kumtumia basi ile rekodi
aliyoiweka kwenye ligi ya kwao atakuja kuiweka na hapa Tanzania.
Suala la viungo kwa jana
walipwaya muda mwingi na kumuacha Tshishimbi akiwa mmiliki halali wa dimba la
katikati, huku Mwalimu Omog akionesha udhaifu wa kushindwa kumwingiza Jonas
Mkude ambaye anaaminika kuwa ndiyo mwenye dimba lake pale katikati. Suala la
mabeki wa simba kujiamini uda mwingi ni zuri lakini kuna muda lilitaka
kuwagharimu na kama si umahiri wa mlinda mlango Aishi Manula basi huenda
shughuli ingeisha mapema.
Simba imekuwa na bahati
ya kupata mabeki wa pembeni wazuri na siku ya jana Ally Shimari na Erasto Nyoni
walionesha kiwango cha juu kabisa. Hivyo ni wito wangu kwa benchi la ufundi
kulifanyia kazi tatizo la umaliziaji hasa kwa Mavugo. Kama atatengenezwa vizuri
basi msimu huu kiatu cha dhahabu itakuwa ni halali yake huku kila aina ya kombe
likiishia mikononi mwa Simba.
Na Shaabani Maulidi #MaulidiTV
No comments