Header Ads

ZIJUE SIMBA NA YANGA KUELEKEA MCHEZO WA KESHO.

Image result for yanga taifa

Na Shaaban Maulidi  #MaulidiTV

Hayawi hayawi yamekuwa sasa na asiye na mwana aeleke jiwe, tambo za hapa na pale zimetawala kuelekeo mchezo wa leo jumatano tarehe 23 agosti 2017 pale uwanja wa taifa jijini Dares salaam pambano la watani wa jadi SIMBA dhidi ya Yanga katika dimba la Taifa majira ya  saa 11jioni, lakini je wajua kuhusu timu hizi…

Unapozungumzia soka la Tanzania huwezi kuacha kuvitaja vilabu viwili vya Simba na Yanga. Hizi ndizo timu kubwa na kongwe kwa hapa Tanzania, na ukubwa wake unajidhihirisha katika majina yake lakini si majina tu bali hata rekodi za timu hizo kitaifa na kimataifa ndizo zinaifanya timu hizo kuonekana ni kubwa mpaka kufikia hatua ya kuitwa Vigogo wa soka la Tanzania. Kila zinapokutana timu hizi lazima Dar es salam isimame na Tanzania kwa ujumla macho na masikio huelekezwa mahali ambapo miamba hii ya soka la Tanznaia hukutana.Image result for yanga imewasili dar


Historia za timu hizi zinafahamika mahala pengi sana duniani lakini naomba nikujuze juu ya historia na rekodi ambazo zimewekwa na vilabu hizi pale zinapokutana lakini kabla ya kufika huko naomba kwanza uzifahamu timu hizi japo kwa ufupi.
Dar es salaam Young African Sports Club maarufu kama YANGA watoto wa jangwani ni klabu ya Tanzania yenye maskani yake katika mitaa ya Twiga na Jngwani Kariakoo jijini Dar es salaam, inayotumia uwanja mkuuwa taifa kama uwanja wake wa nyumbani ni moja kati ya klabu mbili  kubwa zaidi Tanzania huku hasimu wake akiwa ni Simba. Ilizaliwa Februari 11 mnamo 1935 ndiyo inayoongoza kuchukua mataji mengi ya Ligi kuu Tanzania bara tangu kuanzishwa kwake ikiwa tayari imejiwekea kibindoni idadi ya mataji 27 huku hasimu wake akiambulia mataji 18 mpaka hivi sasa. Pia imewahi kuchukua mataji kadhaa ya kimataifa kama vile Kagame cup mara 5 mwaka 1975, 1993, 1999, 2011, 2012.

Image result for yanga taifa
Yanga inayovalia jezi za rangi ya njano na kijani imewahi kuwa na wachezaji nguli kama vile SHAABAN NONDA, MAULIDI DILUNGA, SUNDAY MANARA NA KASSIM MANARA NA SAIDI MAULIDI. Ambao walicheza kwa mafanikio makubwa sana na kubaki kama watu nmashuhuri klabuni hapo. Kwa sasa klabu hiyo inanolewa na kocha Mzambia George Lwandamina, akisaidiwa na mchezaji na nahodha wa zamani wa klabu hiyo Shadrack  Nsajigwa, huku kocha kocha wa makipa akiwa Juma Pondamali, mwenyekiti wa klabu hiyo ni Yusuph Manji ambaye kwa sasa anasota rumande na nafasi yake ikikaimiwa na Clement Sanga wakati Charles Boniface Mkwasa akiwa katibu mkuu na msemaji wake ni Dismas Ten. YANGA ndiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara pia ina idadi kubwa ya wapenzi na mashabiki.

SIMBA SPORTS CLUB maarufu kama WEKUNDU WA MSIMBAZI ni moja kati ya klabu kubwa mbili nchini Tanzania, huku pia jina lake likiwa kubwa barani Afrika kutokana na rekodi ambazo imewahi kuziweka. Timu hiyo yenye maskani yake Mitaa za msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam, ilizaliwa mnamo mwaka 1936 ikijulikana kama Queens, baadaye Eagles, kisha Dar Sunderland na ilipofika mwaka 1971 ikabadili jina na kuwa SIMBA jina linalotumika hadi hivi sasa. Timu hiyo yenye idadi kubwa yawapenzi na mashabiki inatumia uwenja mkuu wa taifa kama uwanja wake wa nyumbani huku ikiwa katika harakati za ujenzi wa uwanja wake binafsi huko Bunju njje kidogo ya jiji la Dar es salaam inayovalia jezi za rangi nyekundu na nyeupe.
Image result for simba taifa

Kuhusu mafanikiao Simba ndiyo Klabu yenye mafanikio makubwa kimataifa licha ya miaka kadhaa ya hivi karibuni kushindwa kushiriki katika mkichuano hiyo kutokana na kushindwa kufanya vizuri ligi kuu Vodacom Tanzania bara. Mnamo mwaka 1993 iliweza kuitoa kimasomaso Tanzania baada ya kutinga kwa fainali ya kombe la shirikisho barani Africa na kufungwa na timu ya Stella club. Pia mnamo mwaka 2003 Simba iliishangaza dunia baada ya kuwang’oa mabingwa wa Africa wa ngazi ya vilabu ZAMALEK YA MISRI na kutinga hatua ya makundi.
Image result for simba taifa 2017

Sambamba na hayo simba imeshaweka kinindoni makombe 18 ya ligi, makombe 5 ya Ligi ya Tasker, na makombe 6 ya ligi ya mabingwa Afrika mashariki maarufu kama kagame Cup. Rekodi nyingine kubwa iliyowekwa na simba ni kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kutolewa na klabu ya GHAZL AL MEHALLA ya MISRI. Kwa sasa timu hiyo inanolewa na Kocha Mcameroon Joseph Omog akisaidiwa na Mganda Jackson Mayanja, Adam Abdallah akiwa ni kocha wa makipa, msemaji wake wa sasa ni Haji Sunday Manara ana SAalim Abdallah anayekaimu nafasi ya Rais Evans Aveva ambaye yupo rumande akikabiliwa na tuhuma kadhaa na makamu wake Goefrey Nyange maarufu kama KABURU. Ndiyo mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho la soka Tanzania maarufu kama Azam sports Federation Cup. Simba pia ipo katika mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa timu kwa hisa na tayari wanachama wameshabariki mfumo huo.

Baada ya kuzijua klabu hizo sasa tungalie baadhi ya rekodizilizowekwa na timu hizo zilipokutana na kujua nani ni mbabe….

1.      Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba hapo tarehe 07/06/1965 pale ipoibugiza Simba bao 1-0 mfungaji akiwa ni Mawazo Shomvi katika dakika ya 15 ya mchezo.


2. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuibamiza Simba kichapo cha paka mwizi cha 5-0 hapo tarehe 01/06/1968. Kwa kipindi cha takribani miaka 9 hivi Simba ilikuwa ikijipanga kulipa kisasi hicho na ilipofika tarehe 19/07/1977 iliibamiza Yanga kipigo kikali zaidi cha 6-0.


3. Abdallah Kibadeni wa Simba ndiye mchezaji pekee aliyeweza kupiga bao 3 (hat trick) katika mapambano ya watani siku ya kifo cha karne cha Yanga cha bao 6-0 siku ya tarehe 19/07/1977. Kipigo hiki hakijalipwa na Yanga hadi leo.


4. Simba kwa mara nyingine tena iliibamiza Yanga kipigo kikali cha bao 5-0 siku ya tarehe 06/05/2012. Kipigo hiki ni malipo kwa Yanga kwa kipigo kama hicho cha tarehe 01/06/1968.

5. Mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizo ulichezwa Februari 25 2017 Ni Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2 – 1 magoli ya simba yakifungwa na Laudit Mavugo na Shiza Kichuya huku goli la Yanga lilifungwa na Simon Msuva.

Jumatano tarehe 23 Agosti 2017 Rekodi nyingine inaenda kuwekwa katika mchezo wa ngao ya jamii katika dimba la taifa Simba ikiwa bingwa wa kombe la Azam Sports Federation Cup huku Yanga ikiwa ni bingwa wa Vodacom Premier League ikiwa ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara pia mchezo huo unatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yakeb aada ya usajiliwa vilabu hivyo wakati Yanga ikiwa imesajili nyota kadhaa kama vile Rostand Youth, Gadiel Michel, Raphael , Pappy Kabamba Tshishimbi na IbrahimAjib watani wao wa jadi Simbawao  wamemsajili Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Emmanuel Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima. .

MSHAIRI MMOJA ALIWAHI KUSEMA
Aungurumapo Simba, Atatetemeka Yanga,
Yanga naye anatamba, Simba kwenda kumfunga,
Rai mimi nawaomba, amani yetu kuchunga,
Kila la kheri wa Simba, Kila la kheri kwa Yanga.

KILA LA KHERI KATIKA MCHEZO HUO AMANI NA UTULIVU ITAWALE
MAKALA HII IMAENDALIWA NAKUSOMWA NA MIMI NI SHAA’BAN MAULIDI.

0718526159 /  0763902318

No comments

Powered by Blogger.