Header Ads

SUP SIO KILEMA


Sup kwangu si kilema, ni matokeo ya kitaaluma,
Kama kusoma nilisoma, mitihani nikajibu vema,
Moduli zote zilituama, imenitokea haijaniuma,
Sup Sio Kilema, tunasapua Tunasepa

Sup ipo UDOM, Mzumbe hadi SAUT,
Sup ipo UDSM, Makumira hadi NIT,
Sup ipo na MUM, hadi Mtwara ya SAUT,
Sup Sio Kilema, tunasapua Tunasepa

Sup ipo kwa walimu, madaktari na mafamasia,
Sup ipo kwa mahakimu, hadi wale mainjiania,
Wahasibu na Masikomu, wanasiasa na wanasheria,
Sup Sio Kilema, tunasapua Tunasepa.

Yawahenga nayakumbuka, leo kwangu kesho kwako,
Wewe unayenicheka, kesho ni zamu yako,
Usijione umekamilika, UE sio mjomba wako,
Sup Sio Kilema, tunasapua Tunasepa

 Tuunde na makundi, kwa pamoja tujadili,
Hata sisi hatupendi, Imetokea kama ajali,
Tulihudhuria vipindi, Biology na Kiswahili,
Sup Sio Kilema, tunasapua Tunasepa

Wapo waajiriwa, walisup wakasapua,
Wapo wahemishiwa, walisup wakasapua,
Wanasup sije pagawa, Semista ijayo tutatoboa,
Sup Sio Kilema, tunasapua Tunasepa

Wala usije jificha, ukasingizia eti spesho,
Huo uoga jaribu acha, ili usisup tena kesho,
Iwe semina iwe lekcha, jitahidi kuvuja jasho,
Sup Sio Kilema, tunasapua Tunasepa

Si kilaza si kipanga, yote amepanga Mungu ,
Tena Sup Sio ujinga, nisikilizie Rafiki yangu,
Tena Sup wala si janga, nitapata degree yangu,
Sup Sio Kilema, tunasapua Tunasepa.

Na Shaaban Maulidi
0718526159/ 0763902318


No comments

Powered by Blogger.