Header Ads

OKWI: SIMBA TUNA TATIZO KATIKA UMALIZIAJI


Mshambulaji wa klabu ya Simba raia wa Uganda Emannuel Okwi amesema timu yao bado ina tatizo la ushambuliaji hivyo wanahitaji kulifanyia kazi.

Akizungumza na Mtilah Blog jana muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa ngao ya jamii kati ya Simba na Yanga Okwi alisema, licha ya ushindi walioupata kwenye mchezo huo lakini safu yao ya ushambuliaji bado imeonekana haiko vizuri.

"ukiangalia maeneo ya ushambuliaji bado tuna kazi kubwa ya kufanya" Alisema okwi alipoulizwa shemu gani ya timu imeonekana kuwa dhaifu.

Okwi alisema kwamba watahakikisha wanalifanyia kazi eneo hilo ili kuweza kuwa sawa. 

Zaidi angalia video hii hapa chini kusikiliza alichosema

No comments

Powered by Blogger.