Header Ads

YANGA YABADILI GIA UUZWAJI WA JEZI, SASA KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA IJUMAA.


UONGOZI wa Yanga umeitisha mkutano na wafanyabiashara wote wa jezi utakaofanyika Ijumaa wiki hii makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.

Ofisa Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Dissmas Ten amesema katika taarifa ya leo jioni kwamba pamoja na kuitisha mkutano huo, wanapiga marufuku mara moja kwa mtu yeyote kuuza jezi yenye nembo ya klabu hiyo kuanzia kesho.

“Yanga inatoa tahadhari kwa watu wote ambao kwa namna moja au nyingine watashiriki kuuza  au jezi zenye nembo ya Yanga kuanzia kesho watakamatwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,”imesema taarifa hiyo.
Ten amesema kwamba kikosi maalum kimeandaliwa kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa jambo hilo na kwamba wahujumu wote watakamatwa.
Hatua hii inamaanisha sasa Yanga wanaelekea kuanza kujiendesha kibiashara, baada ya muda mrefu wa kushindwa kutumia fursa ya rasilimali watu iliyonayo kujinufaisha kimapato. 

No comments

Powered by Blogger.