Header Ads

MNYAMA SIMBA AWASILI RASMI DAR KUJA KUITAFUNA YANGA.

Kikosi cha Simba kimeondoka mjini Unguja kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Watani hao wanakutana Jumatano katika mechi ya Ngao ya Jamii kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini.

Simba imeondoka na kikosi chake kamili, ukiwa ni mwendo wa dakika 20 tu kuvuka bahari ya Hindi hadi jijini Dar es Salaam, jiji kubwa zaidi lililo Mashariki mwa Tanzania Bara.

WACHEZAJI WA SIMBA WAKIINGIA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA ZANZIBAR TAYARI KWA SAFARI YA KWENDA DAR ES SALAAM.

No comments

Powered by Blogger.