Header Ads

MABASI YA ABIRIA KUFUATILIWA NA MFUMO MPYA POPOTE LITAKAPOKUWA.



Leo August 21 2017 Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni na Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani wamefanya ziara kwenye miradi miwili mmoja wa kuanzisha kamera katika maeneo ambayo ni hatarishi kwenye barabara.
Mradi mwingine  ambao wameutembelea ni mradi wa kufuatilia mwenendo wa mabasi na malori barabarani ambao .
Mradi huo uko chini ya SUMATRA kwa kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani watakuwa na chumba cha mawasiliano ambacho kitawawezesha kuona mienendo ya mabasi yote ambao yatakuwa yamesajililiwa rasmi na kuwekwa kwenye mfumo huo.
Mpaka sasa mfumo huo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi ya abiria umefungwa kwenye baadhi ya mabasi ambapo pale utawezesha kufahamu mwendokasi wa basi hilo kuanza mwanzo wa safari yake mpaka mwisho wa safari.

No comments

Powered by Blogger.