Header Ads

SIMBA YA MAMILIONI ILIVYOMSHANGAZA SURE BOY.

Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
BAADA ya kutoka suluhu na Simba, kiungo mshambuliaji
 wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amefunguka
 licha ya usajili wa Simba kutumia mabilioni ya shilingi 
lakini timu hiyo imekuwa na uwezo mdogo uwanjani.
Simba inatajwa kutumia jumla ya Sh bilioni 1.3 katika 
usajili wake wa msimu huu na kupelekea kuwa kikosi 
ghali zaidi kikiwa na mastaa mbalimbali akiwemo
 Emmanuel Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima.
Sure Boy ameyasema hayo kufuatia kutoka sare ya
 bila kufungana na timu hiyo katika mchezo wa 
Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Jumamosi kwenye
 Uwanja wa Azam Complex ulipo Chamazi nje kidogo la Jiji la Dar.


Akizungumza nasi Sure Boy alisema kuwa 
hakutarajia wapinzani wao kucheza katika 
kiwango cha kawaida kama ilivyotokea kwa 
kuwa wana timu inayodaiwa kusajiliwa kwa pesa nyingi.


“Mechi haikuwa rahisi na wala haikuwa ngumu 
sana ila tunashukuru kwa matokeo ambayo 
yametokea, tulijipanga kushinda mchezo wa leo (juzi) 
lakini haikuwa bahati kwa sababu ukiangalia sisi 
ndiyo tulikuwa bora zaidi ya wenzetu na tulistahili kushinda.
“Simba naweza kusema imecheza kwenye kiwango
 cha kawaida sana kwa sababu tumemiliki mpira
 na kufanya mashambulizi ya maana zaidi yao, 
ndiyo maana nasema ya kawaida kwani imekuwa
 tofauti na thamani yake inayosemwa,”alisema Sure Boy.

No comments

Powered by Blogger.