Header Ads

SHAIRI: HUYU NDIYE MREMBO WA UDSM "PASUA KICHWA"


SALOME WA UDSM
SHAABAN MAULIDI
TABORA TANZANIA

Jina lake ni Salome, bint wa mzee Lyimo,
Kitabu changu nisome, yeye kwangu kama somo,
Shahidi Sam Kameme, kweli yaliyomo yamo,
Uwapi wangu Salome, basi rudi UDSM.

Wa Arusha siyo Tanga, mimi wake Sweet Mangi,
Mbalamwezi yake mwanga, pink ndiyo yake rangi,
Ananyonga ni kinyonga, kama ringi yeye haringi,
Uwapi wangu Salome, basi rudi UDSM.

Zimenoga zake lipsi, zimenona zake Hipsi,
Anang'ara kama Chipsi, ni mtamu kama Pepsi,
Mashavuni ana Dimpsi, chuchu zake kama Tipsi,
Uwapi wangu Salome, basi rudi UDSM.


Nilikwona tu kwa Sago, sikukwona kwa Sumbay,
Sketi zako za mitego, kumshinda hata Ney,
Hutumii mikorogo, kama ya Kigosi Ray,
Uwapi wangu Salome, basi rudi UDSM.

Nkamuliza Antonia, mpaka kaka Kamili,
Nkamuliza Sofia, na rafiki yako Lili,
Semina za Historia, na lekcha za Kiswahili,
Uwapi Wangu Salome, basi Rudi UDSM.

Ndo upo kwa Diamond, kuimbwa na Rayvani,
Au ndo kwa Mau_Fund, Maufundi kitandani
Ama Eric Omond, Sang'ombe ndo jina gani?
Au kwa Yamoto Band, wakupwelepweta ndani,
Uwapi Wangu Salome, basi Rudi UDSM
 .
Jina langu Shaabani, ukipenda Maulidi,
Wewe kwangu ni kidani, cha dhahabu ndo zawadi,
Maua kwenye bustani, nakuchuma we waridi,
Kipimo chako wastani, siyo joto si baridi,
Uwapi Wangu Salome, basi Rudi UDSM.

Mwisho natuma salamu, uishi maisha mema,
Bado kwako nina hamu, uwe wangu mke mwema,
Nikupende kwa nidhamu, nikupeleke kwa mama,
Uwapi Wangu Salome, basi Rudi UDSM.


Itaendelea..


Na Shablil President
Wa Nyamwezi Kingdom
2017 Kamilisha Malengo

0718526159/0718526159

No comments

Powered by Blogger.