Header Ads

UEFA IMEREJEA TENA NA UHONDO WAKE, HUKU PSG IKIWA ROHO JUU JUU





Ligi ya Mabingwa Ulaya imerejea, sasa ni msimu wa 2017/18,
 vigogo wote watakuwa uwanjani leo na kesho, beki wa PSG
, Thiago Silva ameenda mbele zaidi kwa kusema presha ni
 kubwa kikosini kwao kutokana na usajili uliofanyika.
Silva anasema ujio wa Neymar na Kylian Mbappe utawafanya
 wawe na presha kubwa kwa kuwa watu wengi watahitaji 
mambo makubwa kutoka kwenye timu yao ambao inatarajiwa
 kukipiga dhidi ya Celtic katika michuano hiyo.
PSG ipo nchini Scotland kwa ajili ya mchezo huo, ambapo 
wababe hao wa Ufaransa, Paris Saint-Germain watakuwa
 na nia moja tu ya kupata ushindi kwa kuwa mastaa 
waliosajiliwa ni w agharama kubwa.“Tumeshasahau
 yaliyopita katika msimu uliopita, tumejiandaa vizur
i kwa ajili ya mchezo huu na muhimu ni kupata
 paointi tatu,” alisema beki huyo wa kati.
Ratiba ya michezo ya leo Jumanne ambayo yote itaanza saa 3:45 Usiku ni hii hapa
Celtic v PSG
Benfica v CSKA
Manchester United v Basel
Olympiakos Piraeus v Sporting CP
Bayern München v Anderlecht
Chelsea v Qarabağ
Roma v Atlético Madrid
Barcelona v Juventus
Ratiba ya kesho Jumatano
Maribor v Spartak
Tottenham v Borussia Dortmund
RB Leipzig v Monaco
Feyenoord v Manchester City
Shakhtar v Napoli
Real Madrid v APOEL
Liverpool v Sevilla Anfield
Porto v Beşiktaş

No comments

Powered by Blogger.