HII NDIYO SABABU YA RAIS MAGUFULI KUMTEUA KAIMU JAJI MKUU
Rais John Magufuli amefichua
siri ya kumteua Profesa
Ibrahim Juma kuwa Kaimu
Jaji Mkuu akisema hakuwa
na historia ya kutosha ya
majaji wengi alipoingia madarakani.
Amesema alipoingia madaraka
ilikuwa kipindi kifupi ambacho
aliyekuwa Jaji Mkuu,
Mohamed Chande Othman
alistaafu hivyo ilimlazimu
achukue muda mrefu wa
kujiridhisha na alitumia
Ibara ya 118 (4) kumteua Kaimu Jaji Mkuu.
Rais Magufuli amesema
hayo leo Jumatatu, Ikulu jijini
Dar es Salaam wakati wa
kumwapisha Jaji Mkuu,
Profesa Juma baada ya
kumteua jana Jumapili.
Hafla hiyo imehudhuriwa na
viongozi mbalimbali akiwemo
Makamu wa Rais, Samia
Suluhu Hassan na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Nilifanya hivi si kwa sababu
hakuna majaji au walikuwa
hawafai, majaji wote ni
wazuri na mnafanya kazi
nzuri sana lakini sikutaka
kuteua jaji baada ya mwaka
mmoja nateua tena au
baada ya miaka miwili anastaafu,
nilitaka nikiteua akae miaka
hata 10, awe ‘anatujaji’ wote
tutakaokuwepo,” amesema Rais Magufuli.
Amesema kumteua Jaji Mkuu
ni kazi ngumu, lazima ujue historia
na tabia zake, pia kuangalia iwapo
ataweza kuendana na dhamira
yake ya kupambana na rushwa.
Rais Magufuli amesema rushwa
ipo kila sehemu, hivyo baada
ya kuchaguliwa na wananchi
mwaka 2015 alikaa chini
na kumwomba Mungu apate
kiongozi atakayeenda kulisimamia
jambo hilo kwa kipindi kirefu zaidi.
Amesema wapo majaji wengi
na wenye sifa lakini baadhi yao
wamebakisha muda mchache kustaafu.
“Katika kufanya uchambuzi
wangu nikamwona Profesa
Juma ambaye alikidhi vigezo
vyangu. Nakupongeza s
ana Profesa Juma ni
Mungu ambaye amekuchagua
kwa hiyo, kawatumikie vizuri
watu wa Mungu na utangulize
mbele masilahi ya Watanzania,” amesema.
Rais Magufuli amesema ingawa
bado kuna changamoto mbalimbali
katika Mhimili huo, alimuhakikishia
Profesa Juma kwamba Serikali
inazitambua na aliwataka majaji
kutembea kifua mbele kwa
kuwa Serikali inatambua kazi
nzuri wanayoifanya.
Amesema kazi nzuri yoyote
haikosi watu wa kuiponda,
akitumia msemo wa mti
wenye matunda ndiyo
unaopopolewa kwa mawe.
Kiongozi huyo mkuu wa
nchi amesema alipomteua
kuwa Kaimu Jaji alipondwa
lakini alikuwa mvumilivu na
hakupata shinikizo la mtu
yeyote la kumteua Jaji Mkuu.
No comments