Header Ads

KILICHOMUONDOA ANCELOTTI BAYERN HIKI HAPA...

 Image result for CARLO ANCELOTTI


Baada ya kukubali kichapo cha magoli 3 -0 kutoka kwa mabingwa wa nchini Ufaransa PSG klabu ya soka ya Bayern Munich imemtimua kocha wake Muitaliono Carlo Ancelotti.

Magoli ya Dani Alves, Edison Cavan na Neymar JR, yalitosha kabisa kuisambaratisha Beyern iliyokuwa ugenini nchini Ufaransa katika mchezao wa ngazi ya makundi ya Klabu bingwa Ulaya usiku ya Jumatano.

Kwa sasa klabu hiyo iytakuwa chini ya aliyekuwa msaidizi wake, Willy Sagnol ambaye  atakuwa kocha wa Bayern Munich kwa muda.

Bayern chini yake, ilionekana kutokuwa na mwendo mzuri sana ingawa iliendelea kushinda mechi kadhaa mfululizo. Hata hivyo katika msimu huu, mwendo wa Bayern haukuwa mbaya ingawa uongozi ulionekana kutofurahishwa na aina ya uchezaji.

CHINI YA ANCELOTTI KWA MSIMU WA 2017-18
Dortmund 2-2 Bayern Munich (Super Cup)
Chemnitzer 0-5 Bayern Munich (German Cup)
Bayern Munich 3-1 Bayer (Bundesliga)
Werder Bremen 0-2 Bayern Munich (Bundesliga)
Bayern Munich 3-0 Anderlecht (Champions League)
Bayern Munich 4-0 Mainz (Bundesliga)
Bayern Munich 2-2 Wolfsburg (Bundesliga)
PSG 3-0 Bayern Munich (Champions League)

No comments

Powered by Blogger.