Header Ads

MANJI ASEMA YEYE BADO NI DIWANI AKIWA MAHAKAMA


Image result for MANJI YUSUPH

MFANYABIASHARA Yusuf Manji 
ameieleza Mahakama ya Hakimu 
Mkazi Kisutu leo September 9, 2017 
kuwa yeye bado ni Diwani wa Kata ya 
Mbagala Kuu na kudai kuwa hatambui
 kuvuliwa udiwani kama ilivyotangazwa
 na Mstahiki Meya wa Temeke,
 Abdallah Chaulembo September 6, 2017.

Manji ametoa malalamiko hayo, kwenye kesi 
ya uhujumu uchumi inayomkabili na wenzake
 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma
 Shaidi ambapo katika kesi hiyo ambayo 
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa
 Kishenyi amedai upelelezi haujakamilika na 
Manji kudai ameona habari kupitia gazetini 
kuwa amevuliwa udiwani.

Amedai kama ni kweli amevuliwa Udiwani 
hatambui, kwani ana miezi 2 yupo gerezan
i na serikali inatambua kwamba yeye ni Diwani.

“Vikao vya awali vya udiwani wa Halmashauri 
ya Temeke nilikuwa nahudhuria kwa kuwa
 naheshimu Mahakama na kwa uzito wa hii
 kesi sikutaka kupeleka hata maombi y
a dhamana Mahakamani.

“Mahakama imuagizie DPP na aiambie 
Halmashauri ya Temeke kwamba
 wamenikamata na ndio sababu 
ya kutohudhuria vikao. Kama wanataka
 nihudhurie DPP aombe remove order 
nitolewe gerezani ili niende kwenye vikao.”

Pia Manji amedai kuwa kama hilo
 haliwezekani, basi wamuandikie 
barua itakayoonyesha agenda
 ya vikao vyote na yeye atazijibu
 kwa njia ya barua pia.

“Ninachotambua mimi ni Diwani
 wa Mbagala Kuu na kama
 nimevuliwa au sijavuliwa
 udiwani sitambui. Tayari nimetumia
 fedha zangu mwenyewe zaidi ya 
Tsh. Milioni 70 sio za Halmashauri 
kwa ajili maendeleo ya wananchi wake.”

Aidha, amedai kuwa hiyo kesi ni nzito
 na DPP hapaswi kuangalia upand
e wake wa kesi tu, kwani yeye
 amechaguliwa na wananchi na anawasaidia.

Awali kabla ya kuelezwa hayo, Wakili 
wa utetezi Seni Malimi alidai kuwa
 wanatarajia kuwasilisha maombi 
ambayo ni ya siri katika tarehe ijayo.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu 
Huruma Shaidi akautaka upande 
wa mashtaka kuhakikisha 
wanalifanyia kazi suala hilo
, ambapo kesi imeahirishwa 
hadi September 18, 2017.

No comments

Powered by Blogger.