Header Ads

JEZI YA TSHISHIMBI YAWA LULU

Image result for PAPPY TSHISHIMBI YANGA







 JEZI za kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi 
tayari zimeanza kuuzwa kwa kiwango cha juu 
mkoani Njombe ikiwa ni siku chache kabla
 ya Yanga haijacheza na Njombe Mji 
kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani humo. 

Njombe Mji na Yanga zinatarajiwa kupambana 
keshokutwa Jumapili ukiwa ni mchezo wa
 Ligi Kuu Bara ambapo Tshishimbi tayari
 ameshajizolea umaarufu kutokana na
 kiwango kikubwa alichokionyesha
 kwenye mechi yake ya kwanza hapa
 nchini dhidi ya Simba katika Ngao ya Jamii. 

Jana Alhamisi,  tulizipata picha
 mbalimbali zikionyesha 
wafanyabiashara wa jezi
 katika Stendi Kuu ya Mabasi Njombe. 

Licha ya kuwepo kwa jezi nying
i za wachezaji mbalimbali wa 
Yanga, lakini zenye jina la
 Tshishimbi raia wa DR Congo,
 ndizo zilikuwa nyingi huku
 ikisemekana kwamba ndizo
 zilizokuwa zikinunuliwa kwa wingi.  

No comments

Powered by Blogger.