Header Ads

SIMBA PASUA KICHWA YAIPASUA HARDROCK 5 - 0, MO MASHINEEEEEEE

Image result for simbA 2017

























Klabu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam jioni ya leo imeshuka dimbani katika uwanja wa Uhuru Chang'ombe Temeke Dar es salaam kumenyana vikali na Klabu ya soka ya Hardrock kutoka visiwani Pemba katika pambano la krafiki ikijiandaa na mchezo wake wa ligi utakaochezwa mwishoni mwa juma lijalo.

Simba ambayo katika mchezo wa leo imewakosa nyota kadhaa wanaotumikia timu zao za taifa, imewatumia wachezaji wengine waliobaki huku wengi wakiwa ni wale waliosajiliwa msimu huu. Simba imefanikiwa kuwafunga maafande wa Hardrock kwa magoli 5 -0.Image result for SIMBA VS HARDROCK


Kwa siku ya leo unaweza kusema kuwa nyota wa mchezo huo ni Mohamed Ibrahim MO Cabaye huku mimi nikipenda kumuita MO MASHINE baada ya kutupia goli 2 kambani, magoli mengine ya Simba yalifungwa na Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto pamoja na mshambuliaji mpya wa klabu hiyo raia wa Ghana Nicholaus Gyan.

Ushindi huo wa Simba unaendeleza ubabe wa klabu hiyo ambayo kwa msimu huu inaonekana kudhamiria kufanya vizuri katika kila mechi huku ikionekana kushusha vipigo vikubwa vikubwa kwa kila wanayekutana naye.
Image result for SAID NDEMLA 2017 SIMBA DAY

Hadi sasa Simba imeshawafunga Gulioni FC magoli 5 - 0, ikamfunga hasimu wake Yanga kwa changamoto ya mikwaju ya Penalti 5 - 4, Mtribwa Sugar ikachezea kichapo cha goli 1 - 0, Ruvu Shooting akila goli 7 - 0, Rayon Sports ya Rwanda ikalala goli 1 - 0 katika mchezo wa Simba Day huku ikishinsdwa kufurukuta mbele ya Mlandege ya Zanzibar baada ya kutoa Suluhu ya 0 - 0.

No comments

Powered by Blogger.