Header Ads

HAZARD AMLILIA COSTA CHELSEA

Eden Hazard amesema angependa kuona Diego Costa akisitisha uamuzi wake wa kubaki Brazil na kurejea Chelsea.

Straika huyo wa kimataifa wa Hispania amekosekana kwenye kikosi cha Chelsea kwa muda mrefu na kushindwa kurejea kwenye maandalizi ya msimu mpya ya klabu hiyo ( Pre-Season )  mwezi Julai , ameachwa kwenye kikosi cha UEFA cha Blues.

Hazard ambaye amecheza mechi zote za kimataifa za Ubeligiji katika kipindi hiki baada ya kupona jeraha lake la kifundo cha mguu anatamani kuona Diego Costa anasitisha mpango wa kugoma kucheza na kurejea kikosini.

"Diego na Mimi tumekuwa tukicheza pamoja kwa miaka mitatu , tumeshinda kila kitu pamoja kasoro UEFA tu "

"Ni raha sana kucheza na yeye, ni mchezaji wa daraja la juu sana na mtu mzuri sana, ningependa kumuona akirejea lakini mimi sifanyi maamuzi."

"Ni matumaini yangu atafute ufumbuzi na kurejea uwanjani kusakata soka.

No comments

Powered by Blogger.