Header Ads

UEFA YAZIKINGIA KIFUA PSG NA MAN CITY

Baada ya barua kutoka Shirikisho la soka nchini Hispania kulitaka shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) kuzichunguza klabu za PSG na Manchester City  kuhusu ukiukwaji wa sheria za matumizi ya fedha, Financia Fair Play (FFP), Hatimae UEFA wamekataa maombi hayo.

Javier Tebas
Rais wa La Liga, Javier Tebas ametoa malalamiko kuhusu wamiliki wa klabu ya Manchester City ambao pia ni wamiliki wa klabu ya PSG kutokana na matumizi makubwa ya kifedha yaliyofanywa na klabu hizo kwenye usajili msimu huu.
Lakini baadaye shirikisho la soka la UEFA limetoa majibu kuhusiana na barua iliyoandikwa na Rais wa La Liga kwa kusema kwamba shirikisho hilo halitaichunguza klabu hizo kwa sasa na taarifa nyingine kinyume na hapo ni uongo mpaka mwishoni mwa msimu.

No comments

Powered by Blogger.