Header Ads

NIYONZIMA AFUNGUKA JINSI SIMBA ITAKAVYOBEBA UBINGWA MSIMU HUU

Image result for niyonzima



KIUNGO wa Rwanda na  Simba, Haruna
 Niyonzima,  amesema moja ya maleng
o aliyojiwekea ni kuhakikisha timu hiyo 
inatwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho
 Afrika hapo mwakani.Simba ilikata tiketi
 ya kushiriki michuano yaKombe la Shirikisho 
Afrika baada ya kuibuka mabingwa wa Kombe
 la FA msimu uliopita

Kiungo huyo aliyejiunga na Simba msimu 
huu akitokea Yanga, alisema ubora wa 
kikosi chao ndio unaomfanya aamini 
wana kila sababu ya kubeba taji hilo.
“Simba tuna kikosi bora msimu huu ndiyo
 maana nawaza ubingwa wa Afrika, naamini
 inawezekana kwa sababu ya aina ya 
wachezaji na kama tutajituma hakuna
 kitakachoshindikana,” alisema Niyonzima.


Niyonzima alisema licha ya ubora
 wa kikosicha Simba kwa sasa,
 anaamini yeye binafsi ana bahati
 ya kuzipa mafanikio timu mbalimbali 
alizowahi kuzichezea tangu akiwa
 nchini  kwao Rwanda na baada ya
 kutua Tanzania.Alisema anatambua
 haitakuwa kazi rahisi, lakini kiu ya 
mafanikio waliyokuwa nayo msimu
 huu anaamini itawasaidia kufikia
 malengo.Hata hivyo, pamoja na 
kuichezea timu yake ya zamani ya 
Yanga kwa miaka mitano, Niyonzima
 hakuwahi kufanikiwa kutwaa 
ubingwa wowote wa michuano ya Caf.

No comments

Powered by Blogger.