Header Ads

MCHEZAJI BORA WA LIGI AKAA BENCHI MECHI MBILI MFULULIZO

Image result for TSHABALALA MOHAMED HUSSEIN 2017 MCHEZAJI BORA


                                     
Mohamed Hussein "Tshabalala"            
AMA kweli hakuna ufalme unaodumu milele! 
Beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’
 alikuwa kama mfalme wa nafasi ya 
kushoto msimu uliopita pale Simba na
 aliweka rekodi ya kucheza mechi zote 
za ligi, lakini mambo yamebadilika msimu
 huu, amepata mpinzani na amepigwa 
benchi mechi mbili mfululizo kwenye ligi.
Juzi Simba ilicheza dhidi ya Azam FC
kwenye Uwanja wa Azam Complex, 
Chamazi jijini Dar na kutoka suluhu. 
Tshabalala alikuwa benchi.

Tshabalala hadi sasa ameshindwa kufua
 dafu mbele ya beki mpya wa timu hiyo, 
Erasto Nyoni ambaye amejiunga na
 klabu hiyo hivi karibuni akitokea Azam FC.

Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, 
Joseph Omog amekuwa akimpatia Nyoni 
nafasi ya kucheza kila wakati kutokana na 
kuonyesha uwezo mkubwa tangu alipojiunga
 na timu hiyo.

Akimzungumzia mchezaji huo, Omog alisema:
 “Nyoni ni mchezaji mwenye faida kubwa anapokuwa 
uwanjani, mbali ya kucheza nafasi ya beki wa 
kushoto lakini pia ana msaada mkubwa kwa mabeki 
wa kati na pindi tunapokuwa tunashambuliwa.
“Anajua kukaba vizuri lakini pia anajua kuanzisha
 mashambulizi, kwa hiyo ni mtu muhimu sana katika kikosi changu.
“Kuhusu Tshabalala ni mchezaji mzuri lakini siwezi 
kuwatumia wote kwa pamoja ila atacheza tu, mechi bado ni nyingi.”

No comments

Powered by Blogger.