Header Ads

KAULI YA KOCHA WA MTIBWA BAADA YA SULUHU NA YANGA.



Siku ya Jumamosi ya tarehe 30 Septemba ulipigwa mchezo wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara kati ya Mabingwa mara 27 wa kombe Yanga SC hilo dhidi ya mabingwa mara 2 wa kombe hilo Mtibwa Sukari ya mkoani Morogoro uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya bila bila kufungana ambapo timu hizo zimegawana pointi moja moja. Baada ya mchezo huo kocha wa Mtibwa Sukari Zuberi Katwila ameuzungumzia mchezo huo..

***“Mechi ilikuwa ngumu ukizingatia tunacheza na Mabingwa watetezi na sisi tulikuwa tunaongoza Ligi na wao walikuwa wanatafuta namna ya kupata point tatu, sisi tulikuwa ugenini na tumetafuta ushindi lakini imeshindikana tumepata sare”*** Katwila

No comments

Powered by Blogger.