Header Ads

VIJANA CHANGAMKIENI FURSA – MAVUNDE

Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,

Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
 Mh.Anthony Mavunde jana alikuwa mgeni 
rasmi katika uzinduzi rasmi msimu wa 
FURSA 2017 mkoani Arusha.

“Tumehutubia sana,tumesema sana, tumejadili 
sana,tumepanga mipango sana, sasa ni wakati
 wa kuachana na dhana hii na kutenda, kufanya,
 na sio kufanya tu bali kufanya kweli” ..
Ni maneno alionena kwa hisia kali Naibu Waziri 
Anthony Mavunde akizungumza na mamia ya
 vijana na vikundi mbalimbali mkoani Arusha
 Tanzania katika muendelezo wa msimu wa 
FURSA 2017.

Naibu Waziri Mavunde aliwataka Vijana 
kuhakikisha wanatumia fursa ya Mifuko 19 
ya Uwezeshwaji Wananchi Kiuchumi kama 
sehemu ya kupatia mitaji ya shughuli 
mbalimbali za kiuchumi na hivyo kusaidia 
kuondokana na masharti magumu ya 
Taasisi za Fedha nyingi.

Aidha pia, Aliwashukuru sana timu nzima
 ya Fursa chini ya muasisi ndg.Ruge Mutahaba
 kwa kuzidi kuisaidia jamii ya kitanzania na
 serikali kwa ujumla wake kufanikisha maendeleo 
ya nchi hii na kuonesha kwa vitendo dhana nzima ya ushirikishwaji.

Mgeni Rasmi ndugu Mavunde aliizungumzia 
dhana hii ya Fursa na kauli mbiu yake mwaka
 huu ya Anzia Sokoni akiwataka vijana na 
watanzania wote wanaotaka kufanikiwa 
kutokata tamaa na kuwa na malengo 
yenye tija, kuhakikisha kila siku wanaitumia
 kuwaza jambo la kufanya na la kuwaletea maendeleo.
Pia,alizungumza ni namna gani serikali mpaka 
sasa imefanya katika kuhakikisha ina watengenezea 
vijana mazingira bora na kukazania kwenye mipango
 iliyopo kwao kuanzia wale walio katika mfumo rasmi
 wa elimu na wale walionje ya mfumo kuwatengenezea
 mazingira ya kuendeleza shughuli zao mfan
o useremala,ushonaji nk kuwapa mafunzo na kuwatengeneza kua bora.


Mwisho aliwashukuru washriki wa Fursa 2017 Umoja wa 
mataifa kwa kuendelea kushika ajenda hii ya vijana ikiwa 
kwa mkoa wa Arusha kupitia ILO wanaendelea kutoa 
mafunzo ya uanagenzi kwa vijana,pia Letshego Tanzania
 kwa kujidhatiti kuwasaidia vijana kwa mikopo na 
sapoti nafuu pia ushauri katika safari yao ya 
kujikwamua kimaisha,wadau wengine ni wazara 
ya Afya na kampeni yao ya NIPO TAYARI 
wakihimiza usafi hasa wa maliwatoni kunawa mikono.
Kuelekea kuhitimisha Mh Mavunde alikubaliana 
na mtazamo wa FURSA 2017 wa Anzia Sokoni 
akithibitisha kua katika lolote lile lazima kujua soko linataka nini.

No comments

Powered by Blogger.