Header Ads

KATIBU MKUU WA CHADEMA AJISALIMISHA POLISI


Katibu Mkuu wa Chadema, 
Dk Vincent Mashinji ameamua
 kwenda kuripoti Makao Makuu
 ya Jeshi la Polisi jijini Dar

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu
 na Mkuu wa Idara ya Habari
 na Mawasiliano ya Chadema,
 Tumaini Makene imesema 
Dk Mashinji ameambatana
 na wasaidizi wake kutoka
 makao makuu ya chama hicho.

“Katibu mkuu amewasili Makao 
Makuu ya Jeshi la Polisi,
 jijini Dar es Salaam,
 kuitikia wito wa Polisi
 uliotolewa na Kamanda 
wa Polisi Mkoa wa Dodoma,
 Gilles Muroto, kuwa anatakiwa
 kufika Ofisi ya Mkurugenzi
 wa Upelelezi wa Makosa
 ya Jinai (DCI)” amesema.

Awali, leo Jumatatu Dk Mashinji 
alisema  hawezi kwenda kuripoti
 kwa kuwa hakuambiwa siku
 maalumu ya kwenda.

Kamanda Muroto amemtaka 
Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi
 wa Makosa ya Jinai mkoani 
Dodoma au ofisi kama hiyo
 iliyopo Kituo Kikuu cha Polisi 
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
 ili kutoa ushirikiano kwa jeshi 
hilo kuhusu tukio la kushambuliwa
 kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

“Nina taarifa za kuitwa Polisi,
 lakini haziko ‘specific’.  
Ni wakati wowote naweza
 kwenda? na hawajasema 
nikaripoti wapi. Kwa hiyo, 
wakinihitaji watakuja kuniambia,
” alisema Dk Mashinji leo asubuhi. 
Lissu alipigwa risasi na watu
 wasiojulikana Septemba 7
 mchana alipokuwa akielekea
 nyumbani kwake Area D mjini Dodoma. 
Kwa sasa Lissu anaendelea 
na matibabu katika Hospitali
 ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya.

No comments

Powered by Blogger.