Header Ads

MGODI WA MWADUI WAFUNGWA


\
Uongozi  wa Kampuni  
ya Williamson Diamonds Limited
 (WDL) umesitisha  kwa muda
 baadhi ya shughuli za uzalishaji 
 katika mgodi huo.

Taarifa ya uongozi wa mgodi
 huo kwa wafanyakazi 
jana, zilisema huduma
 za uzalishaji zimesimamishwa
 isipokuwa huduma maalumu 
 za ulinzi, tiba, umeme, maji,
 zimamoto na usafiri  unaohitajika
 katika huduma hizo.

Taarifa hiyo ilisema huduma za
 utawala  zitaendelea  
kufanya kazi wakati huduma 
nyingine zitakazoendelea 
kuendeshwa na mgodi
 itatolewa taarifa   uzalishaji
 utakaporejea.

Taarifa hiyo  ilisema Kampuni
 ya WDL  inasubiri agizo la 
 kuacha kusafirisha nje 
almasi yake  kutoka mgodini,
 kifurushi namba W1-FY18.

Hata hivyo, taarifa za ndani
 zinasema Serikali imezuia 
kusafirisha kifurushi hicho 
kwa misingi ambayo haijawasilishwa
 rasmi kwao licha ya kuona taarifa
 hizo kupitia vyombo vya habari.

“Hatuwezi kutoa maoni yoyote
 kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.

“Vifurushi vyote vinavyosafirishwa 
kwa biashara nje hukadiriwa thamani 
yake hapa mgodini na watumishi 
wa ‘TANSORT’ ambacho ni kitengo 
cha kukadiria thamani ya almasi 
na vito  wanaowawakilisha 
Wizara ya Nishati na Madini.

“Kifurushi kinavyosafirishwa 
kinapigwa mihuri miwili ya
 vyombo viwili vya Serikali,
 sisi uongozi hatuna ujuzi 
wanaoutumia ‘TANSORT’ 
wa kukadiria kwa muda
 malipo ya mrabaha kwa Serikali.

“Yanakamilishwa  baada ya 
kupatiwa matokeo halisi ya 
zabuni ya wazi ya almasi za 
WDL  na uaminifu wake
 unathibitishwa na TANSORT 
kutoka wizarani,’’ilieleza 
sehemu ya taarifa hiyo.

Kamishna wa Nishati na Madini,
   Benjamin Mchwampaka jana 
alisema taarifa ya mgodi huo 
haijafika kwake   bali ameiona 
kwenye mitandao ya  jamii.

Alisema mpaka sasa hawezi 
kujua athari za kusimamisha 
uzalishaji wa mgodi huo  hadi 
  atakapopata taarifa rasmi
 kutoka kwa uongozi.

“Nimeziona mitandaoni, 
sijapata taarifa kutoka 
kwao wenyewe itabidi 
kuitafakari ikifika kesho (leo).

“Lazima niweze kujua 
hilo na niweze kufahamu 
pia athari na wamefunga  
maeneo gani na athari 
hata kwa wafanyakazi 
itakuwa kwa kiasi gani ,
’’alisema  Mchwampaka.

Hivi karibuni wafanyakazi 
wa Uwanja wa Ndege 
wa Kimataifa wa Julius 
Nyerere (JNIA),   walikamata 
mzigo wenye madini ya almasi 
yenye uzito wa kilo 29, dakika
 tano kabla ya ndege kupaa,  
huku yakiwa yameandikwa yana kilo 14.3.

Inaelezwa walioshiriki kufanya 
udanganyifu huo  ni watumishi 
wa serikali  waliopewa dhamana 
 ya ukaguzi na uthaminishaji 
katika mchakato wa kuanzia
 mgodini hadi kuidhinisha 
usafirishaji wa madini hayo nje ya nchi.

Waziri wa Fedha na Mipango,
 Dk.Philip Mpango, juzi alitembelea 
uwanja wa JNIA kwa ajili ya kutoa 
maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa 
Mashitaka (DPP), Mganga Biswalo.

Alisema Tanzania imepigwa vya 
kutosha hivyo   wote waliohusika
 katika udanganyifu huo washughulikiwe 
kwa mujibu wa sheria.

Waziri alisema wafanyakazi wote
 waliohusika kuanzia hatua ya
 uchimbaji wa madini hayo 
mpaka kule yanakosafirishwa,
 wamulikwe  na vyombo 
vya dola  kubaini uhalali wa 
mali zao wanazomiliki.

Ilielezwa kuwa  wamiliki wa 
mgodi wa madini hayo walisema
 yana thamani ya Dola za 
Marekani milioni 14.8, lakini 
baada ya uchunguzi ilibainika  
  thamani yake ni  Dola za 
Marekani milioni 29.7.

No comments

Powered by Blogger.