Header Ads

MAASKOFU WATOA TAMKO KUHUSU LISSU KUSHAMBULIWA

(TEC), limelaani shambulizi la hivi
 karibuni lililotekelezwa na watu 
wasiojulikana dhidi ya Mbunge 
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mbunge huyo aliyejeruhiwa Septemba 7 
kwa kupigwa risasi tano mjini Dodoma, 
hivi sasa anaendelea na matibabu 
katika Hospitali ya Aga Khan, 
jijini Nairobi nchini Kenya.

Baraza pia limeungana na Watanzania
 kulaani kwa nguvu zote matendo yote
 ya vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani nchini.

Tamko la baraza hilo lililosainiwa na
 Makamu wa Rais wa TEC, Askofu 
Beatus Kinyaiya limetolewa baada 
ya kikao cha kawaida cha baraza
 kilichofanyika kwa siku mbili Septemba
 9 na 10 jijini Dar es Salaam.

“Katika Taifa letu sasa tunashuhudia
 matendo ya mauaji ya watu wasio 
na hatia kama ilivyokuwa kule Mkuranga,
 Rufiji na Kibiti, utekwaji wa watu na kuteswa, 
utekaji wa watoto, ulipuaji wa ofisi za watu na
 hivi karibuni shambulio la mbunge Lissu,”
 limesema baraza katika tamko hilo.

Imeelezwa vurugu na mashambulizi ya 
aina yoyote ile yanalifedhehesha Taifa 
kwa kuwa matendo hayo ni dhambi, 
uhalifu na si utamaduni wa Mtanzania, 
hivyo vyombo vinavyohusika havina budi 
kuyakomesha mara moja.

No comments

Powered by Blogger.