Header Ads

SIMBA HAIWEZI KUSHINDA BILA YA OKWI: TAMBWE

Image result for AMIS TAMBWE


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga,
 Mrundi, Amissi Tambwe, amefurahishwa
 na matokeo ya bila kufungana ambayo 
Simba iliyapata juzi Jumamosi ilipocheza 
na Azam FC.

Hata hivyo, Tambwe ambaye msimu wa 2013/14
 alikuwa akiitumikia Simba, alisema kuwa 
alijua kabisa timu hiyo isingepata matokeo 
mazuri katika mechi hiyo bila ya uwepo wa
 Mganda, Emmanuel Okwi kwenye mchezo huo.

Akizungumza nasi Tambwe alisema kuwa
 kwa washambuliaji wa Simba waliopo hivi
 sasa, ukimwondoa Okwi, ilikuwa ni ngumu 
kwao kuifunga Azam kutokana na kutokuwa
 na ubunifu wa kutafuta ushindi pindi wanapokuwa 
wamebanwa vilivyo na mabeki wa timu pinzani.

Emmanuel Okwi.
“Matokeo hayo nimeyapokea vizuri na nimefurahi 
baada ya kuona kile nilichokuwa nikiwaza 
akilini kwangu kimetimia, kwani nilijua kabisa
 Simba wangekutana na matokeo hayo katika mchezo huo.

“Hiyo ni kwa sababu washambuliaji wengi wa timu
 hiyo siyo wabunifu wa kutafuta mbinu mbadala za
 kufunga pindi wanapokuwa wamebanwa vilivyo na wapinzani wao.
“Mchezaji pekee ambaye angeibeba Simba katika 
mechi hiyo alikuwa ni Okwi lakini baada ya kusikia
 tu kuwa hatacheza mechi hiyo moja kwa moja 
matokeo hayo waliyopata yakanijia akilini kwangu,
” alisema Tambwe na kuongeza:

“Kwa hivyo hivi sasa dalili ya sisi kuchukua 
ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya nne mfululizo 
nimeanza kuiona na ninamwomba Mungu nirejee 
mapema uwanjani ili niweze kuisaidia timu yangu
 ya Yanga kutimiza ndoto yetu hiyo.”
Image result for EMMANUEL OKWI 2017 NGAO YA JAMII

No comments

Powered by Blogger.