Header Ads

YANGA HAITAKI MCHEZO KABISA YAMLETA MRITHI WA BOSSOU

BEKI wa SM Sanga Balende ya mjini Kinshasa, DR Congo, Fiston Kayembe anayedaiwa kuwa ndiye atakayerithi mikoba ya Vincent Bossou kwenye kikosi cha Yanga, ameonekana kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kayembe alifika mazoezini hapo akiwa ameongozana na kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi na kuangalia mazoezi ya kikosi hicho chini ya kocha George Lwandamina.
Beki huyo ambaye anatarajiwa kujaribiwa na benchi la ufundi kwa muda wa wiki mbili na akifanya vizuri atasainishwa mkataba wa awali na kurejea klabuni kwake kumalizia mkataba wake uliobakiza miezi michache.

Akizungumzia kuwapo kwa beki huyo, kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, alisema hawajatambulishwa kuhusu mchezaji huyo.

“Sijajua kama kuna mchezaji mgeni, ila tupo tayari kumsimamia yeyote yule kwa kuwa ndio kazi yetu, hayo mambo mengine wanajua viongozi,” alisema Mwandila.

Yanga imemleta Kayembe ili kumrithi Bossou ambaye hakuongeza mkataba mpya, baada ya klabu kushindwa dau alilolitaka nyota huyo ili kuongeza mkataba mpya.

No comments

Powered by Blogger.