Header Ads

WAZIRI MKUU MSTAAFU AMJULIA HALI TUNDU LISSU
















Waziri Mkuu wa zamani, Edward 
Lowassa yupo Nairobi nchini
 Kenya kumjulia hali Mbunge
 wa Singida Mashariki, Tundu 
Lissu aliyelazwa katika Hospitali 
ya Aga Khan, baada ya kushambuliwa 
kwa risasi na watu wasiojulikana.

Lissu ambaye pia ni mwanasheria
 wa Chadema alijeruhiwa kwa
 risasi tano Alhamisi Septemba 7
 akiwa ndani ya gari nyumbani
 kwake Area D mjini Dodoma 
akitokea bungeni.

Katika akaunti yake ya Twitter, 
Lowassa ame-tweet akisema,
 “Earlier today i paid a visit at 
Nairobi Hospital to see our 
MP, President of TLS and 
dear friend @tundulissutz 
He is recovering well.
 It is Sad times for Tanzania.
 Let us all keep praying.”

Kwa tafsiri isiyo rasmi amesema
 “Mapema leo nilitembelea 
Hospitali ya Nairobi  
kumwona mbunge, 
Rais wa Chama cha Wanasheria 
wa Tanganyika (TLS) na 
rafiki kipenzi Tundu Lissu.
 Anaendelea vizuri. Ni kipindi
 cha masikitiko kwa Tanzania.
 Kwa pamoja tuendelee kuomba.”

Katika tweet hiyo, Lowassa 
ambaye ni Mjumbe wa Kamati 
Kuu ya Chadema, ameweka
 picha akiwa pamoja na Alicia
 ambaye ni mke wa Lissu; 
Mwenyekiti wa Chadema, 
Freeman Mbowe na dereva
 wa Lissu Simon Mohamed Bakari.

No comments

Powered by Blogger.