Header Ads

SOMA SHAIRI LA GAUNI LA KUAZIMA UPATE BURUDANI NA ELIMU.

GAUNI LA KUAZIMA
SHAABAN MAULIDI
TABORA TANZANIA
Ugeni si kitu chema, ugenini we chutama, 
Kubali kutenda wema, kubali beba lawama,
Asiyefunzwa na mama, atafundishwa na umma,
Gauni la kuzimaliza, kuazima kunaponza.
Kisikia sikukuu , wewe roho juu juu,
Hautaki kuu kuu, unataka vipya tuu,
Hataki bei nafuu, majuto ni mjukuu,
Gauni la kuanzia, kuazima Kuna pona.
Hautaki vitu vyako, watamani vya wenzako,
Sikukuu zote zako, kuazima fani yako,
Hata hutulii kwako, Kila siku sokomoko,
Gauni la kuanzia, kuazima kunaponza.
Yakuwasha pilipili, ijapokuwa hauili,
Mwili wako nyulinyuli, kama taa ya chemli,
Kama kijiko hoteli, ama siti kwa nauli,
Gauni la kuazima, kuazima kunaponza.
Mara ukaombe dera, tena zuri siyo baya,
Mara ukaombe dira, hujisikii vibaya,
Unaruka kama chura, wa majungu na umbeya,
Gauni la kuanzia, kuazima kunaponza.
Mungu amekupa nguvu, hutaki kufanya kazi,
Unaendekeza uvivu, kudandia tu mavazi,
Umejawa na uchovu, kucha kutwa matembezi,
Gauni la kuazima, kuazima kunaponza.
Unaomba hadi wanja, cha ajabu na hereni,
Unajiona mjanja, waomba hadi sabuni,
Wajua vyote viwanja, kama gari la kampeni,
Gauni la kuazima, kuazima kunaponza.
Unapenda kunywa bia, hujawahi kulipia,
Melewa kupindukia, matusi unayatoa,
Hutaki jihidumia, kuna siku utalia,
Gauni la kuazima, kuazima kunaponza.
Na juzi umeumbuka, baada ya kujisifia,
Na nguo ulojivika, wamekuja kukuvua,
Aibu umeaibika, ukabaki unalia,
Gauni la kuanzia, kuazima kunaponza.
Mwanamke kujiremba, jirembe kwa vya kwako,
Hata kama vya mtumba, huo ndo uwezo wako,
Sakafuni utaramba, sipoenda mwendo wako,
Gauni la kuazima, kuazima kunaponza.
Na Shablil President
Wa Nyamwezi Kingdom
0718526159/0763902318
2017 Kamilishamalengo

No comments

Powered by Blogger.