Header Ads

MATOKEO YA MICHEZO YA UEFA ILIYOPIGWA JANA. ,MESSI AMEVUNJA REKODI HII



Michezo nane ya ufunguzi hatua ya Makundi
ya michuano ya UEFA Champions League
msimu wa 2017/2018 imechezwa usiku wa
Jumanne ya September 12 2017 barani Ulaya,
FC Barcelona wamecheza mchezo wao wa
 kwanza dhidi ya Juventus ya Italia katika
uwanja wa Nou Camp.

Barcelona wakiwa katika uwanja wao wa
 Nou Camp wameendeleza rekodi yao kwa
 kucheza mchezo wao wa 23 wa UEFA 
Champions League hatua ya Makundi
katika uwanja wake wa nyumbani pasipo
 kupoteza wakiwa wametoa sare game mbili pekee.

Lionel Messi leo kwa mara ya kwanza amefanikiwa kumfunga golikipa wa Juventus Gianluigi Buffon akicheza dhidi yake mara nne baada ya kufanikiwa kumfunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-0, magoli akifunga dakika ya 45 na 69 baada ya Ivan Rakitic kuifungia Barcelona goli la pili dakika ya 56.

Matokeo ya game zote nane za UEFA Champions
 League zilizochezwa usiku wa September 12 2017.

No comments

Powered by Blogger.