Header Ads

KIPA ALIYEDAKA SIMBA DAY AMEFARIKI DUNIA


















Ulimwengu wa soka leo umepata pigo jingine
baada ya kumpoteza mchezaji wa kimataifa wa
 Ivory Coast aliyokuwa anaichezea Beijing
Enterprises Cheick Tiote, leo zimeripotiwa
 habari za kufariki kwa golikipa wa club ya
Rayon Sports ya Rwanda Evariste Mutuyumana.

Golikipa wa Rayon Sports Evariste Mutuyumana
amefariki dunia baada ya kupata tatizo la kushindwa
 kupumua vizuri, kama utakumbuka vizuri Evariste
Mutuyumana ni miongoni mwa wachezaji wa Rayon
 waliyokuja Tanzania kucheza na Simba katika
 mchezo wa Simba Day.

Evariste Mutuyumana
Evariste Mutuyumana ndio golikipa wa Rayon
Sports aliyedaka katika mchezo wa Simba Day
 August 8 2017 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam
 na Simba kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0
 lililofungwa na kiungo wao Mohamed Ibrahim
dakika ya 16.

No comments

Powered by Blogger.