Header Ads

BUNGE LAMUAHIDI USHIRIKIANO JAJI MKUU MPYA





Spika wa Bunge la Tanzania, 
Job Ndugai amefunguka na kudai 
atahakikisha yeye na wabunge wanampa
 ushirikiano Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis 
Juma aliyeapishwa leo baada ya kuteuliwa
 siku ya jana Septemba 10 mwaka huu.

Ndugai ametoa kauli hiyo wakati
 alipokuwa anatoa salamu za 
wabunge katika ghafla hiyo ya
 uapisho iliyofanyika katika 
viwanja vya Ikulu Jijini 
Dar es Salaam na kuhudhuriwa
 na viongozi mbalimbali wa 
kitaifa bila ya kumsahau 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

"Sisi kama bunge tunawahakikishia
 ushirikiano mkubwa sana kwa
 kuhakikisha kazi za Mahakama
 zinaendelea kama zilivyo kikatiba
 na tutaheshimu sana. Yale 
maneno na makombora moja
 moja ya bungeni ni vitu vya
 kawaida, ndiyo utamadun
i wa bunge",amesema Ndugai.

Aidha, Ndugai amesema
 Mahakama inamchango
 mkubwa kwa wananchi
 pamoja na taifa kwa
 ujumla kwa kuwa hicho 
ndicho chombo 
pekee kinachoweza 
kumtetea mnyonge 
kuweza kupata haki
 yake kutoka kwa waporaji.

"Kuwepo kwa Mahakama
 ndiyo usalama wetu,
 amani, kheri na matumaini 
ya mnyonge katika sheria
 na maamuzi ya Mahakama.
 Kwa hiyo tunakutakia kila 
la kheri katika kazi yako,
 tunakuombea kwa
 Mwenyezi Mungu
 na tutakusaidia na
 kuomba msaada wako",amesisitiza Ndugai.

Kwa upande mwingine, 
Jaji Mkuu Prof. Ibrahim
 Hamis Juma ameahidi 
kufanya kazi katika
 maadili ya kisheria pamoja
 na kurudisha imani ya 
wananchi kuhusiana na
 kupata misaada ya
 kisheria inayotolewa 
katika Mahakama mbalimbali
 ndani ya Tanzania

No comments

Powered by Blogger.