Header Ads

OMOG HANA PRESHA NA MECHI YA AZAM KESHO

Image result for OMOG
BENCHI la ufundi la Simba chini ya kocha wake mkuu, Joseph Omog, raia wa Cameroon, limeweka wazi kuwa licha ya mch­ezo wao dhidi ya Azam FC kuhamishiwa kwenye Uwanja wa Azam Com­plex ambao unamilikiwa na wapinzani wao hao, lakini suala hilo halitaon­doa suala la wao kupata matokeo mazuri ambayo wanayataka.
Simba, kesho Jumamosi kwa mara ya kwanza watacheza na Azam kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ndani ya Uwanja wa Azam Complex baada ya mch­ezo huo kuhamishwa kutoka Uwanja wa Uhuru ambapo ulipangwa mara ya kwanza.
Mcameroon huyo amesema kuwa hawana presha na suala hilo la kwenda kucheza Azam Com­plex kutokana na yeye kuujua uwanja huo kutokana na ku­fanya kazi miaka ya nyuma pia kwenye soka la kisasa lolote linatokea haijalishi timu in­acheza kwenye uwanja gani.
“Hapana, hatuna presha ya kucheza kwenye uwanja wa wapinzani wetu hao kwa sababu tumejipanga kupata pointi na tuna wachezaji wanaoweza kulitimiza hilo, lakini kwenye soka hili la kisasa haijalishi ni wapi ambapo utakuwa unacheza kama umejiandaa vya kuto­sha wewe ndiye utaibuka na pointi,” alisema Mcameroon huyo.

No comments

Powered by Blogger.