BREAKING: Madini ya Bilioni 32 yazuiwa kusafirishwa Airport DSM (+video)
Leo September 1 2017 Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, ACP Martin Otieno amekutana na wanahabari ili kutoa taarifa kuhusu mzigo wa Almasi ambao umezuiwa usisafirishwe kwenda nje ya Tanzania.
Kamanda Otieno amesema “tumezuia mzigo wa almasi ambao ulikuwa usafirishwe jana kuelekea ubelgiji, almasi hizo zilikuwa zinatoka mgodi wa Mwadui Shinyanga, tumeuzuia ili kujua thamani halisi baada ya thamani iliyotumika kutiliwa mashaka’
‘Tunatilia mashaka hii thamani ya Bilioni 32.8 kwa sababu ina maana tayari Serikali itakuwa imepata mrahaba mdogo katika gawio la hisa hii’-ACP Martin Otieno
TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI KUFAHAMU ZAIDI
Chanzo cha habari hii ni millardayo.com
No comments