Header Ads

MECHI YA SIMBA SASA NI JUMAPILI

Mchezo wa kirafiki kati ya Simba sc na klabu ya Hard Rock ya kisiwani Pemba uliokua umepangwa kupigwa leo jioni katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam umesogezwa mbele, sasa utapigwa Jumapili ya Tarehe 03, septemba

Hii nikutokana  na uwanja ulipangwa kwa mchezo huo ambao ni uwanja wa Uhuru kutumiwa na timu ya Taifa ya Botswana katika mazoezi ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania(Taifa Stars).
Kwa mujibu wa klabu ya Simba kupitia akaunti yake rasmi ya Instagram imeweka wazi kuahirishwa kwa mchezo huo na kuweka bayana kua pambano hilo limesogezwa mbele kutoka tarehe 1 hadi tarehe 3 ambayo ni siku ya Jumapili.

No comments

Powered by Blogger.